Habari/News

Mnyika atuma salamu kwa wabunge wa Chadema waliopo rumande

Tarehe December 6, 2017

John Mnyika, Mbunge wa Kibamba akichangia hoja bungeni.

Wakati wabunge wawili wa Chadema, Peter Lijualikali (Klombero) na Susan Kiwanga (Mlimba) na madiwani wawili na wanachama 34 wakiendelea kusota rumande kwa tuhuma za kufanya fujo na kuchoma ofisi ya mtendaji, Mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika ametumia ukurasa wake wa Facebook asubuhi hii kuongea machache kuwahusu.

Viongozi hao na wanachama hao wa Chadema wanatuhumiwa kufanya fujo hizo na kuchoma ofisi ya mtendaji baada yakutangazwa matokeo ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Sofi, Wilayani Malinyi.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Mnyika ameandika yafuatayo;

“Nasimama na wabunge wetu wawili; Ndugu Peter Lijuakali na Susan Kiwanga, Madiwani wetu wawili na wanachama wetu 34 ambao kwa mara ya pili sasa bado wanakataliwa kupewa dhamana.

Ikumbukwe walikamatwa toka Novemba 26 mpaka sasa wananyimwa haki yao ya msingi ya kupata dhamana.

Ninaheshimu mhimili wa Mahakama; lakini kwa yaliyowahi kwisha tokea na mifano lukuki inasukuma hitaji la sauti zetu. Kumeshakuwa na njama ovu nyingi dhidi yetu wapinzani hasa ktk suala zima la utoaji wa haki ya msingi ya dhamana-inahitaji kupazwa sauti zetu na kuunganisha nguvu kukemea hili.

Tuungane ktk hili na madhila mengine mengi ya uvunjifu wa haki, demokrasia na usawa ktk kuendesha siasa nchini.

Tunahitaji siasa safi ili tuweze kupiga hatua kimaendeleo kama alivyotuasa Baba yetu, Mwl. Julius Nyerere.

Aluta continua! ✌🏿✌🏿✌🏿.”

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni