Habari/News

Mnyika aibuka kutoka mafichoni, asema haya

Tarehe December 6, 2017

Mbunge wa Kibamba kwa tiketi ya Chadema, John Mnyika.

Mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika hatimaye ameibuka na kukanusha taarifa za kwamba amejiuzulu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Bara.

Mapema jana katika mitandao ya kijamii kulizagaa taarifa za kwamba kada huyo wa Chadema amejiuzulu nafasi hiyo huku kukiwa na barua yenye nembo ya Chadema ikionesha kuandikwa na Mnyika akielezea uamuzi huo.

Mnyika ambaye kwa muda mrefu sana amekuwa kimya na hadi kupelekea kuibuka kwa maswali juu ya kupotea kwake, amelazimika kujitokeza na kukanusha taarifa hiyo hasa baada ya kuwa amekuwa akitajwa tajwa na kuhusishwa na kukihama chama hicho kuelekea Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mnyika amesema taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba amejiuzulu si za kweli, ni taarifa za uongo.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni