Habari/News

Mkuu wa Wilaya aamrisha Kamati ya Ulinzi kuchoma nyumba 900

Tarehe October 12, 2017

Nyumba zaidi ya 900 zimechomwa moto wilayani Chunya kwa amri ya mkuu wa Wilaya Bi. Rehema Madusa akishirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama.

Uamuzi wa kuchoma nyumba hizo unafuatia  madai ya wananchi kuvunja sheria kwa kuvamia na kuishi ndani ya hifadhi ya misitu ya asili iliyopo tarafa Kipembawe Chunya.

Kwa mujibu wa Meneja wa wakala wa huduma za misitu (TFS) Grace Wille, wilaya ya Chunya amesema kuwa katika tarafa ya Kipembawe kuna misitu zaidi ya saba inayohifadhiwa, lakini misitu hiyo imevamiwa na makundi ya watu ambao wanaendesha shughuli za kiuchumi na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira na kwamba zoezi hilo la kuwaondoa ambalo limeanza leo litakuwa ni endelevu.

Nao wananchi waliochomewa nyumba zao wameshangazwa na uamuzi huo kwa madai kuwa maeneo hayo waliuziwa na  viongozi wa vijiji.

Hadi sasa   zaidi ya kaya 1000 zimekosa mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kuchomwa moto.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni