Habari/News

Miili ya watu sita yaopolewa ajali ya Boti Kigoma

Tarehe December 24, 2017

Miili sita ya watu waliozama katika ajali ya boti kugonga mtumbwi katika Ziwa Tanganyika imeopolewa.

Hayo  yamebainishwa na  Ofisa  Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) mkoa wa Kigoma,  Amaniel Sekulu.

Mpaka sasa idadi ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea Ijumaa iliyopita imefikia 19 kutokana na awali kuopolewa miili 13.

Sekulu amesema miili hiyo sita imeharibika kutokana na kukaa majini zaidi ya saa 50 na kuongeza kuwa uopoaji wa miili hiyo ilikumbwa na changamoto kadhaa, ikiwemo wazamiaji kukumbana na hali mbaya ya hewa, mvua za mara kwa mara, mawimbi makubwa na kina kirefu cha maji.

Amesema Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ)  na wananchi wenye ujuzi wa kuogelea ndio waliofanikisha kupatikana kwa miili hiyo. MV Pasaka ilikuwa imebeba waumini wa Kanisa la Pentekoste waliokuwa wanakwenda kwenye mkutano wa injili na sherehe za sikukuu Krisimasi katika kijiji cha Sunuka.

Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia Ijumaa ikihusisha boti la Atakalo mola lililokuwa linatoka Kigoma jini kwenda Kalya na mtumbwi wa MV Pasaka uliookuwa ukitoka kijiji cha Kalilani kwenda Sunuka.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni