Habari/News

Miguna atoka Dubai,asafirishwa kwenda Canada

Tarehe April 2, 2018

Mwanasiasa wa upinzani Miguna Miguna.

Mwanasiasa wa upinzani aliyezuiwa kuingia Kenya wiki iliyopita na kusafirishwa kwa lazima hadi Dubai amewasili nchini Canada.

Miguna Miguna, ambaye ni wakili, alisafiri kwa ndege iliyokuwa ikielekea Toronto, Canada, baada ya kukaa katika uwanja wa kimataifa wa Dubai kwa siku nne.

Mmoja wa mawakili wa mwanasiasa huyo Nelson Havi ameandika kwenye Twitter kwamba Bw Miguna amesafiri kwenda Canada kwa hiari kupitia usaidizi wa ubalozi wa Canada katika Umoja wa Milki za Kiarabu (UAE).

Bw Havi amesema Miguna atafanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na “atarejea baadaye.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni