Habari/News

Mhariri gazeti la The Guardian aokotwa hajitambui Bunju

Tarehe April 8, 2018

Mwandishi ambaye pia Mhariri wa gazeti la The Guardian, Finnigan Simbeye ameokotwa eneo la Bunju wilayani Kinondoni akiwa hajitambui.

Taarifa ya kuokotwa mwandishi huyo  imesambaa leo Aprili 8, 2018 ambapo baada ya kuokotwa alikuwa na  kitambulisho chake cha kazi cha kampuni ya The Guardian Limited.

Akizungumzia tukio hilo Rose Mirondo, ambaye ni mkewe Simbeye amesema mumewe aliondoka nyumbani jana Jumamosi Aprili 7, 2018 akiwa na gari lakini hakurudi hadi alipopata taarifa za kuokotwa kwake leo.

Rose amesema watu aliowakuta eneo la tukio wamemweleza kwamba Simbeye alichukuliwa na polisi kupelekwa hospitali.

Naye kamanda wa polisi Mkoa wa Kinondoni, Murilo Jumanne amesema hana taarifa za tukio la kuokotwa Simbeye.

Mwandishi huyo kwa sasa  amefikishwa Hospitali ya Mwananyamala kwa huduma ya haraka.

 

Kitambulisho cha Mwandishi huyo.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni