Habari/News

Meya Jacob aingilia kati sakata la Mnyika, atoa onyo kali

Tarehe December 5, 2017

Meya Manispaa ya Ubungo, Boniphace Jacob.

Wakati jina la Mhe. John Mnyika ambaye ni Mbunge wa Kibamba kwa tiketi ya Chadema likiendelea kugonga vichwa vya watu katika vijiweni na mitandao ya kijamii juu ya uwezekano wa kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM), Meya wa Ubungo (Chadema), Boniphace Jacob ameingilia kati sakata hilo na kusisitiza kuwa Mnyika hanunuliki.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Meya Jacob ametoa onyo kwa mtu aliyemuita ‘babaenu’ kuacha kuendelea kumpigia simu Mnyika vinginevyo watamuaibisha.

Meya Jacob ameandika maneno yafuatayo;

“TULIENI MNYIKA YUPO KWENYE MIKONO SALAMA

Mwambieni Babaenu aache kupiga simu Ovyo,Tumemrekodi na tutaendelea kumrekodi tumuaibishee……Any time atume sms au apige tena aone!!!!!!!!!
Mnyika siyo Dizaini ya hao unaowapigia simu na kuwahahidi Vyeo na Madaraka ya kuhongwa…..Tunakuweka loudspeaker tunakusikiliza tuh…..ukikata simu tunacheeeeeeeeeeeekaa.

Etiiii unamwambia Binadamu Mwenzako unamtaka kwa gharama yeyote…….ili nini?.”

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni