Habari/News

Lijualikali kuendelea na ubunge licha ya kuswekwa gerezani

Tarehe January 12, 2017

 

Professor-Jay

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bw. Kailima Ramadhan ameweka wazi kuwa Mbunge wa Kilombero Mhe. Peter Lijualikali (30), ataendelea na wadhifa wake huo licha ya kuhukumiwa kwenda gerezani miezi sita (6).

Ramadhan amebainisha hilo kufuatia kuibua kwa mjadala mkubwa wa nini itakuwa hatma ya ubunge wa mfungwa huyo baada ya kumaliza kutumikia adhabu yake hiyo.

Amesema kwamba mbunge huyo ataendelea na wadhifa wake kwa kuwa sheria inasema ili kupoteza kiti ni lazima uwe umepewa adhabu ya kifungo cha zaidi ya miezi sita jela.

“Ibara ya 67(2)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza mambo yanayotoa sifa ya kuwa Mbunge kutoka madarakani ni kifungo cha zaidi ya miezi sita jela. Huyu bwana kafungwa miezi sita kwa hiyo bado hajapoteza sifa za kuendelea kuwa mbunge akiwa gerezani na baada ya kumaliza kifungo chake,” amesema Bw. Kailima.

Mahakama ya Wilaya ya Kilombero jana ilimhukumu kutumikia kifungo cha miezi sita jela bila faini Mbunge wa jimbo la Kilombero Mhe. Peter Lijualikali (30) pamoja na dereva wake, Stephano Mgata (35) kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki katika maeneo ya ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni