Habari/News

Mbunge mwingine Chadema atiwa mbaroni kwa uchochezi

Tarehe November 9, 2017

Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Vincent B. Mashinji.

Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kusini na Mbunge wa Jimbo la Ndanda, Mkoani Mtwara, Cecil Mwambe anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo kwa tuhuma za uchochezi.

Mwambe ambaye hadi sasa anashikiliwa na Jeshi hilo anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi katika mkutano wa kampeniza uchaguzi mdogo wa madiwani zilizofanyika jana Mjini Mtwara.

Kwa mujibu wa Wakili wake, Rainery Songea, Mwambe anatuhumiwa kutoa maneno ya uchochezi katika mkutano wa kampeni ambapo inadaiwa kuwa maneno aliyoyatamka yanasababisha watu kufanya makosa.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni