Habari/News

Mbunge Mwingine CCM atangaza kung’atuka

Tarehe November 9, 2017

Profesa Anna Tibaijuka.

Mbunge wa Jimbo la Muleba Kusini Prof Anna Tibaijuka ametoa ya moyoni kuwa hato gombea tena nafasi ya ubunge  jimbo la Muleba katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2020.

Prof Tibaijuka amesema hayo mkoani Kagera jana na kubainisha kuwa amesha aga kwa wananchi hatagombea tena ubunge katika jimbo hilo katika uchaguzi mkuu ujao kwa kuwa ana mpango wa kustaafu.

Amesema ni wakati sasa wa kuwaachia vijana wafanye kazi kwa kuwa kizazi chake wameshafanya kazi sasa inabidi kupumzika masuala ya siasa.

Wakati Prof Tibaijuka akitarajia kustaafu, hivi karibuni Mbunge wa CCM Lazaro Nyalandu alitangaza kujiuzulu nafasi ya ubunge kwa madai ya kutoridhishwa na uongozi wa Rais Dkt.John Pombe Magufuli pamoja na kushamiri ukiukwaji mkubwa wa Haki za binadamu.

Hata hivyo,baada ya kujiuzulu  Nyalandu aliomba  akaribishwe chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) ambako alifunguliwa milango,

Prof .Tibaijuka amewahi kuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na kung’atuka kutokana na kuhusishwa na sakata la Tegeta Escrow.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni