Habari/News

Mbunge CCM:’Makonda anavunja sheria kuanika mambo ya siri’

Tarehe April 11, 2018

Mbunge wa Ulanga (CCM), Gudluck Mlinga amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda anavunja Katiba kwa kuanika hadharani mambo ya siri jambo ambalo linakwenda kinyume na Katiba .

Akiomba Mwongozo wa Spika Mlinga amelitaka Bunge ambalo ni chombo cha dola kukemea jambo hilo ambalo  ni kinyume na Katiba ya Tanzania.

Mwongozo huo uliibua kelele bungeni baada ya mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga kutoa majibu kwamba suala hilo ni la kisheria.

Hata hivyo wabunge walipinga  na kuhoji sheria ipi imetumika kuhalalisha mpango wa Makonda kuwaita wanawake wanaodaiwa kutelekezwa na wanaume.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni