Habari/News

Mbunge CCM Aula Bunge la Afrika

Tarehe May 11, 2018

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mheshimiwa Stephen Masele.

Mbunge wa Shinyanga Mjini (CCM), Stephen Masele amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP).

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge  amesema   kuwa mbunge huyo kijana amechaguliwa jana kwa kishindo.

“Umelipa Bunge letu sifa na Tanzania kwa ujumla. Nafasi hii ni ya kuitangaza nchi yetu na Bunge hili tunamtakia kazi njema,” amesema Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi (CCM).

“Nampongeza sana kijana huyu, lakini pia Serikali kwani huwezi kupata nafasi hii kubwa kama huungwi mkono na Serikali. Nimpongeze sana Rais John Magufuli.”

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni