Habari/News

Mbunge awahimiza wanaume kuoa wake wengi

Tarehe April 12, 2018

Mbunge Gathoni.

Mbunge mmoja nchini Kenya amefufua tena mjadala wa iwapo wanaume wanafaa kuwaoa wanawake wengi.

Mbunge huyo ambaye ni Gathoni wa Muchomba, mwakilishi wa wanawake kutoka kaunti ya Kiambu, amesema wanaume wakiwaoa wanawake wengi mengi ya matatizo ya kijamii yatafikia kikomo.

Amedai tangu jamii hiyo ilipotupilia mbali utamaduni huo, matatizo mengi yametokea ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaorandaranda mitaani.

Mwaka 2014, Rais Uhuru Kenyatta aliidhinisha Sheria ya Ndoa ambayo inawaruhusu wanaume kuoa wanawake wengi kisheria iwapo watasajili ndoa zao kama za kitamaduni au za Kiislamu.

Aidha, Bi Muchomba alisema wengi wa wabunge tayari wamewaoa wake wengi na “wanajivunia” jambo hilo.

Wakristo hata hivyo hawaruhusiwi kuoa wake wengi chini ya sheria hiyo.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni