Habari/News

Mbowe,Viongozi wengine Chadema wapata dhamana

Tarehe April 3, 2018

Viongozi wa Chadema katika Mahakama y kisutu.

Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe  pamoja na viongozi wengine wa Chadema leo wamepata dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Viongozi hao wote kwa pamoja walitakiwa kila mmoja kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini hati ya dhamana ya Sh20 milioni na kuwa na barua kutoka kwa viongozi wao ama wa vijiji au mtaa, ambao watapaswa kuwa na nakala za vitambulisho vyao.

Viongozi walioshikiliwa ni pamoja na  Katibu Mkuu Dk. Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu.

Kwa upande wa Wabunge  ni Peter Msigwa (Iringa Mjini), John Mnyika (Kibamba), Esther Matiko (Tarime Mjini),pamoja na Halima Mdee Kawe.

Aidha, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee  Mahakamni hapo  amesomewa mashtaka mawili ya kufanya mkusanyiko usio halali na kuendelea na mkusanyiko huo, kutotii amri iliyowataka kutawanyika na kusababisha vurugu iliyosababisha kifo cha Akwilina Akwilini na askari kujeruhiwa.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni