Habari/News

Mbowe amlipua Masha

Tarehe November 16, 2017

Godbless Lema akisalimiana na Lawrence Masha.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa aliyekuwa mwanachama wao, Lawrence Masha hakuwa na msaada wowote ndani ya chama hicho.

Masha ambaye awali alikuwa mwanachama wa CCM kabla ya kuhamia Chadema alitangaza kukihama chama hicho cha upinzani hivi karibuni ikiwa ni miaka miwili tu tangu kujiunga nao.

Kwa mujibu wa Mbowe, kuondoka kwa Masha katika Chama hicho hakujabadilisha kitu chochote bali kumeimarisha chama na kupokea wanachama wengi wapya, hivyo kuondoka kwa mtu asiyekuwa na msaada ndani ya chama hicho si tatizo.

“Alikuwa hatusaidii chochote ndani ya chama, kwani ulishawahi kumsikia amefanya chochote akiwa chadema? acha amfuate babu yake, acha aondoke zake, sisi hatujapoteza chochote, hata alipokuwa waziri alifanya nini, acha aende kwenye biashara zake Uingereza maana tunasikia anawekeza kule,” amesema Mbowe

Masha aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, alitangaza uamuzi wa kuondoka Chadema kupitia taarifa yake iliyosambazwa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ya kuamua kuachana na Chadema huku akisema chama hicho kina safari ndefu ya kuweza kuchukua dola.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni