Habari/News

Maxcom Africa kupunguza  wafanyakazi

Tarehe May 8, 2018

Kampuni ya Maxcom Africa imetangaza kuajiri wafanyakazi wapya wenye ujuzi unaohitajika kutokana na teknolojia kubadilika hivyo kupunguza wafanyakazi wasiohitajika.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Maxcom Africa, Deogratius Lazari  amesema  kwa sasa kampuni hiyo ina watumishi 451 lakini baada ya Serikali kuanza kutumia mfumo wa kielektroniki kwenye masuala mengi mfano utoaji wa zabuni, ukusanyaji wa mapato na maeneo mengine, baadhi ya majukumu yamepungua huku mengine yakizaliwa.

“Huwezi kurundika wafanyakazi wengi kwenye eneo moja bila kujali tija yao. Tulipunguza baadhi ya wafanyakazi walioonekana ufanisi wao upo chini mwaka jana ila awamu hii ni kutokana na mabadiliko ya teknolojia,” amesema Lazari.

Naye mkurugenzi wa uendeshaji wa kampuni hiyo, Charles Natai inasema utaratibu wa kisheria utazingatiwa kufanikisha mchakato huo kwa wafanyakazi watakaolazimika kupunguzwa.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni