Habari/News

Matokeo rasmi uchaguzi wa Ubunge majimbo matatu

Tarehe January 14, 2018

Mtokeo ya uchaguzi katika majimbo matatu yanaonesha kuwa  Chama cha Mapinduzi CCM kimevigalagaza vyama vvya upinzani  na kushinda katika viti vya ubunge katika majimbo matatu  ya Songea Mjini, Longido na Singida Kaskazini.

Jimbo la Longido msimamizi wa uchaguzi, Jumaa Mhina amemtangaza Dkt. Stephen Kiruswa kuwa mshindi baada ya kupata kura 41,258 sawa na 99.1% .

Katika Jimbo la Songea Mjini ambalo lilichwa wazi baada ya mbunge wake Leonidas Gama kufariki dunia

Mgombea wake Dkt Damas Ndumbaro ametangazwa kuwa mshindi kwa kupata kura  45,762 sawa na 97%, huku mgombea aliyemfuatia wa CUF akiwa amepata kura 608, na mgombea wa ADA-TADEA akiwa wamepata kura 471.

Katika jimbo la Singida Kaskazini ambalo lililoachwa wazi na Lazaro Nyalandu aliyejiuzulu wadhifa wake, CCM kupitia mgombea wake mgombea Justine Monko (CCM) imeshinda baada ya kupata kura 20,857 sawa na 93.5%.

Katika uchaguzi huo vyama vya CHADEMA,Act Wazalendo  na CUF vilitangaza kususia.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni