Habari/News

Matokeo kidato cha nne yatangazwa,yatazame hapa

Tarehe January 30, 2018

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde

Jumla ya watahiniwa  385, 767 walisailiwa kufanya mtihani kidato cha nne mwaka 2017, kati yao 287,713 sawa na asilimia 77.09 ndio wamefaulu ambapo wasichana ni  143,728 sawa na asilimia 75.21 na wavulana 143,985 sawa na asilimia 79.06.

Hayo yamesemwa na Katibu Mtendaji wa Necta,  Dk Charles Msonde na kubainisha kuwa  mwaka 2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa 277,283 sawa na asilimia 70.09.

Amesema matokeo ya watahiniwa 50 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya baadhi ya masomo ya mitihani hiyo, watapata fursa hiyo mwaka huu.

Katika mtihani huo Dk Msonde amesema watahiniwa 265 waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani  matokeo yao yamefutwa huku mtahiniwa mmoja akiandika matusi katika karatasi yake ya majibu.

 

    Matokeo Ya Mtihani Wa Kidato Cha Nne (Csee) 2017

Matokeo Ya Mtihani Wa Kidato Cha Nne (Csee) 2017

Matokeo Ya Mtihani Wa Maarifa (Qt) 2017

Matokeo Ya Mtihani Wa Maarifa (Qt) 2017

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni