Habari/News

Marekani yampa onyo kali Raila Odinga

Tarehe December 7, 2017

Rais Uhuru Kenyatta akila kiapo cha Urais.

Marekani imemtaka Kiongozi wa Upinzani nchini Kenya, Raila Odinga kuachana na mpango wake wa kuapishwa kama Rais wa nchi hiyo wiki ijayo.

Onyo hilo linakuja wakati Odinga akiwa anajiandaa kuapishwa Desemba 12, mwaka huu kama Rais wa watu wa Kenya ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu Rais, Uhuru Kenyatta kuapishwa baada ya kushinda kwa kishindo uchaguzi wa marudio ambao ulisusiwa na upinzani.

Uchaguzi wa marudio ulifanyika baada ya Odinga kuwasilisha malalamiko juu ya mapungufu katika uchaguzi mkuu wa awali ambao pia Kenyatta aliibuka kidedea..

Msaidizi wa Katibu wa Masuala ya Afrika Marekani , Donald Yamamoto ambaye ametembelea nchini Kenya ametaka Odinga kuachana na mpango huo na kutaka kufanyika majadiliano ya pande zote mbili kati ya upinzani na serikali iliyopo madarakani.

Baadhi ya viongozi wa serikali wameonya kuwa tukio hilo la kuapishwa linaweza kuhusishwa na uhaini wakati tayari Odinga ameshatoa kadi za mualiko kwa viongozi na watu mbalimbali kwa ajili ya shughuli hiyo.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni