Habari/News

Mapapa ya ESCROW, Rugemarila na Harbinder Seth waburuzwa mahakamani

Tarehe June 19, 2017

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola.

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola.

Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Nchini (TAKUKURU) leo imesema inawashikilia Mkurugenzi wa PAP, Harbinder Sigh Seth na Mfanyabiashara, James Rugemarila kwa makosa ya uhujumu uchumi.

Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Valentino Mlowola amesema hizo ni taarifa za mapambano yao dhidi ya rushwa na ufisadi nchini na kwamba watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kwa makosa hayo ya uhujumu uchumi.

“Tutawafikisha mahakamani kwa makosa ya uhujumu uchumi na makosa mengine yanayofanana na hayo,” amesema.

19225544_1449975981748324_2983678628245640704_n

Amesema kwa muda mrefu amekuwa akiulizwa kuhusiana na wapi kesi za Escrow na IPTL zilipoishia kwakuwa TAKUKURU ina jukumu la kimsingi la kupambana na rushwa na ufisadi.

Tulichunguza shauri hili kwa muda mrefu sana na sasa umefika wakati muafaka wa kuwafikishwa watuhumiwa hawa wakuu mahakamani na tayari tumeshawapeleka mahakamani.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni