Habari/News

Mambosasa :’Mange Kimambi ni Mwenzetu, sasa anaipongeza Serikali’

Tarehe May 11, 2018

Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa  amesema kwamba Mwanaharakati Mange Kimambi sasa ni mwenzao kwa kuwa anaipongeza serikali ya awamu ya tano.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini hapa leo Mambosasa amesema mnamo Aprili 26, 2018 Jeshi la Polisi liliwakamata vijana ambao walikuwa kwenye maandalizi ya maandamano ambayo yalihamasishwa kwa njia ya mtandao na mwanadada Mange Kimambi lakini baada ya kushindwa maandamano hayo Mange  alianza kuipongeza serikali.

“Nawasihi vijana mnaotumia mitandao ya kijamii mnaposhabikia vitu angalieni madhara, yani faida na hasara zake kwani mnamo Aprili 26 tuliwakamata vijana waliokuwa wakijiandaa kwa maandamano ambapo mhamasishaji Mange Kimambi baadae akaanza kuipongeza Serikali. Mange ameendelea kuipongeza serikali nasi tunampongeza kwa kuwa amerudi kundini”, amesema Mambosasa

Amesema Mange Kimambi anapotosha jamii ila watanzania walipompuuza sasa ametambua ni afadhali naye arudi kuipongeza serikali.

Akizungumza kuhusu hali ya usalama amesema  kwa sasa hali ya usalama Jijini Dar es Salaam imezidi kuimarika siku hadi siku

Kuhusu vijana waliokamatwa baada ya kutaka kufanya maandamano yaliyohamasishwa na Mange na Kimambi Mambosasa amesema waliwahoji na kisha kuwapa dhamana.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni