Habari/News

Makonda afichua kilichomvutia Rais Kagame Tanzania

Tarehe January 12, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame anatarajia kuwasili nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ambapo uwezo mkubwa wa Rais Magufuli na Demokrasia ya kweli  vimetajwa   kuwa ni mambo ambayo yamemvutia   kuja Tanzania.

Hayo yamesemwa na  MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam baada ya kuagana na Rais Magufuli ambaye ameelekea visiwani Zanzibar kushiriki sherehe za maadhimisho ya Miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

“Amani Demokrasia ya kweli, upendo na uwezo wa mkubwa wa Rais Magufuli ndiyo msingi wa kuwavuta wageni kuja kutembelea hakuna mgeni ambaye anaweza kutembelea nchi ambayo haina upendo, amani na mshikamano. Tanzania chini ya uongozi wa Rais Magufuli inaendelea kuchanja mbuga katika nyanja za kidemokrasia hasa pia katika uwanja mwingine wa kidiplomasia na kuwafanya wageni waone sehemu nzuri ya kuja kutembelea,” alisema Makonda.

Rais Kagame atawasili nchini siku ya Jumapili ya tarehe 14 ambapo atakuwa nchini kwa ziara ya siku moja na kufanya mazungumzo na Rais John Pombe Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Wakati rais Kagame akitarajia kuwasili nchini,tayari Rais Dkt.John Pombe Magufuli ameshawahi kumtembelea Rais Kagame nchini Rwanda.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni