Habari/News

Makonda aapa kula sahani moja na wanaume waliotelekeza watoto

Tarehe April 12, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuanzia leo atwapigia simu wababa waliotajwa katika sakata la kutelekeza watoto na kuahidi kuwakama endapo watagoma.

Akizungumza na  umati mkubwa wa wamama ambao wamefika ofisini kwake Makonda amesema kwa siku mbili hizi tayari wameshaweza kusikiliza wanawake zaidi ya elfu moja mia nne na kuwataka wamama hao wamepofika ofisini kwake wawe huru na kuongea mambo yote wasiogope wala kupangiwa mambo ya kuzungumza.

“Wale watakao itwa na wakakaidi kuja mimi nitakwenda kuwakamata kwa hiyo wababa niwaombe tu tusipimane ubavu, msipime nafasi yangu kama ina nguvu au haina nguvu na wale wanaotaka mambo ya siri tunza mwanao ndiyo siri pekee”Amesema Makonda.

Kuhusu watu Maarufu Makonda amesema tayari watu mia moja na saba wametajwa hivyo wote wanaatakiwa kufika katika ofisi yake na kuhojiwa.

Amesema watu maarufu wamekuwa wakihitaji kukutana naye chemba au waje ofisi kwa nafasi za pekee hivyo amesema kuwa hataki kukutana na mtu yoyote chemba wala kupigiwa simu bali wanapaswa kufika ofisini kwake

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni