Habari/News

Makamu wa Rais atimkia rasmi Dodoma

Tarehe December 15, 2017

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan atangaza kuhamia Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametangaza kuhamia rasmi mkoani Dodoma kutii agizo la Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

Akizungumza mara baada ya kuwasili nyumbani kwake Kilimani mjini Dodoma, Samia ameomba wananchi wa mkoa huo kuonyesha ushirikiano katika kufanya kazi ili kulisukuma gurudumu la maendeleo.

“Nilikuwa hapa kwa muda mrefu kidogo lakini nilipangiwa kuhamia rasmi leo Desemba 15 na nimefurahi kwamba nitafanya kazi mahala pangu pa kazi pa kudumu,” amesema Samia.

Amesema kauli mbiu yake kwa wakazi wa Dodoma ni kuufanya mji huo kuwa wa kijani hivyo Desemba 21 ataendesha mpango wa kupanda miti katika wilaya zote.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni