Habari/News

Mahakama yampa Lissu onyo la mwisho

Tarehe August 7, 2017

Tundu Lissu akiwa mahakamani.

Tundu Lissu akiwa mahakamani.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imempa onyo la mwisho, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kuhakikisha kuwa anafika mahakamani hapo kujibu mashtaka ya uchochezi yanayomkabili.

Onyo hilo limetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa baada ya wakili wa serikali, Mutalemwa Kishenyi kudai kuwa shauri hilo limekuja kwa ajili ya kusikilizwa lakini mshtakiwa Lissu hajafika Mahakamani.

Wadhamini wa Lissu hawakufika pia Mahakamani huku Wakili wa Lissu, Jeremiah Ntobesya akidai kuwa mteja wake ana hudhuru,

Akitoa onyo hilo, Hakimu Mwambapa amesema hii ni mara ya pili Lissu hajafika katika kesi hiyo hivyo anatoa onyo la mwisho ahakikishe anafika.

Amesema kinyume na hapo, hatua za kisheria zitachukuliwa na kuahirisha kesi hiyo hadi Agosti 14, 2017.

Lissu anadaiwa kutenda kosa hilo Julai 28, 2016 katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Ilala Dar es Salaam, akitumia maneno ya ‘Dikteta Uchwara’

Continue with more paragraphs …

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni