Habari/News

Maalim Seif apata pigo,Sasa kambi yake kukosa Ruzuku

Tarehe August 12, 2017

Maalim Seif.

Maalim Seif.

Hiisasa/ Dar es salaam

Habari kwa ufupi….

Chama Cha Wananchi (CUF) kambi ya Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad imepata pigo jingine kufuatia Mahakama Kuu nchini Tanzania kutupilia mbali pingamizi lao kutaka Profesa Ibrahim Lipumba asipewe ruzuku za chama hicho.

Aidha, Mahakama Kuu imetupilia mbali pingamizi hilo  jana tarehe 11 Agosti 2017, kufuatia Chama Cha CUF huko nyuma kufungua kesi ya msingi ya madai kuhusu wizi wa ruzuku na shauri dogo la kuweka zuio kutolewa kwa ruzuku ya chama kutokana na wizi wa shilingi milioni 369 ambazo zilidaiwa kuibwa na Lipumba na kundi lake kwa kushirikiana na Msajili wa Vyama Vya Siasa.

Kufuatia kesi hiyo  kutupiliwa mbali  kwa sasa Prof. Ibrahim Lipumba ataendelea kupokea ruzuku .

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni