Habari/News

Maadhimisho miaka 56 ya Uhuru kufanyika Dodoma

Tarehe December 7, 2017

Makomandoo wakionesha uwezo wao wakati wa Maadhimisho ya uhuru.

Maadhimisho ya kutimiza miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania bara kwa mwaka 2017  yatakayofanyika Desemba 9, katika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Hayo yamesemwa na  Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Bilinith Mahenge na kubainisha kuwa maonesho hayo yatapambwa na  gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama nchini, onesho la vikosi vya Komandoo, kwata ya kimyakimya na gwaride la mkoloni kutoka Jeshi la Polisi.

Mgeni rasmi katika sherehe hizo za maadhimisho anatarajiwa kuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Kauli mbiu ya Maandhimisho hayo  mwaka huu ni ‘Uhuru wetu ni tunu, tuudumishe, tulinde rasilimali zetu, tuwe wazalendo, tukemee rushwa na uzembe’.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni