Habari/News

Lowassa, Sumaye wamtembelea Lema akijiandaa kuupokea mwaka gerezani

Tarehe December 31, 2016

fb_img_1483178908309

Mawaziri Wakuu wa zamani Edward Lowassa ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema Taifa na Fredrick Sumaye leo wamemtembelea gerezani Mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema kwa lengo la kumsalimia kiongozi huyo.

Wamemtaka Mbunge huyo kutokata tamaa na kuwa dhamana yake itapatikana tu.

Lowassa ameongozana na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Mhe.Kalist Lazaro na Bob Lowassa, hadi Gereza Kuu la Kisongo Mjini Arusha na kumjulia hali Lema.

Lema yupo rumande tangu alipokamatwa mwanzoni mwa mwezi Novemba na hivyo mbunge huyo ataupokea mwaka mpya akiwa gerezani kufuatia kushindikana kwa dhamana yake licha ya jitihada mbalimbali zilizofanywa na mawakili wake.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni