Habari/News

Lowassa: CCM walinibania Urais kwa kutaka kufumua mikataba ya madini

Tarehe June 14, 2017

lowassa-na-bashe

Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa amesema kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kilihakikisha hapenyi katika kinyang’anyiro cha kupata ridhaa ya kugombea Urais kupitia chama hicho tawala kwakuwa dhamira yake ilikuwa kufumua mikataba yote ya madini.

Lowassa amesema hayo alipokuwa akizungumzia sakata la mchanga wa madini (makinikia) na kumpongeza Rais Magufuli kwa hatua anazochukua dhidi ya rasilimali hizo ikiwemo kuagiza kupitiwa upya kwa mikataba ya madini.

“Dhamira yangu wakati natangaza nia ya kuwania urais ndani ya CCM ilikuwa ikijulikana wazi kuwa ni pamoja na kufumua mikataba ya madini na ndio maana walihakikisha sipenyi,” amesema Lowassa.

Wakati huohuo, Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kuanzia sasa endapo Serikali italeta sheria kwa hati ya dharura juu ya sheria za madini, bunge halitapitisha kwa kuwa nchi imeibiwa vya kutosha.

 

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni