Habari/News

Lowassa azidisha utata Chadema kuitisha Kamati kuu Kesho

Tarehe January 12, 2018

Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akiwa na Mwanasiasa Edward Lowassa.

Aliyekuwa mgombea urais wa kwa tiketi ya Ukawa Edwrd Lowassa anatajwa kuongeza utata kuhusu kuitishwa kwa mkutano wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kesho jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Zanzibar, Salum Mwalimu amesema lengo la kikao hicho  ambacho ni cha dharula  ni kufanya tathmini ya hali ya kisiasa nchini.

Hata hivyo,alipoulizwa kama kikao hicho kinahusiana na kujadili ziara ya waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwenda Ikulu, Mwalimu amesema kikao hicho kilipangwa kufanyika Desemba mwaka jana lakini kiliahirishwa kutokana na sikukuu za mwisho wa mwaka.

Amesema licha ya kikao hicho kupangwa ila ajenda ya kumjadili Lowassa huenda  ikawepo.

Amesema ajenda za kikao hicho zilipangwa kabla Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema hajaenda Ikulu hivyo hakina uhusiano na ziara hiyo ila huenda jambo hilo likajitokeza.

Wakati mkutano huo ukiitishwa  hivi karibuni Mwanasiasa Edward Lowassa amezua gumzo kufuatia kufanya ziara ya kwenda  Ikulu ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli na kumpongeza kwa utendaji wake wa kazi.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni