Habari/News

Lissu atoboa siri ya Chadema kumchukua Lowassa

Tarehe January 11, 2017

Edward Lowassa.

Edward Lowassa.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kiliamua kumchukua aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa, ajiunge na chama hicho baada ya kubaini alikuwa na uwezo wa kubeba asilimia 18 ya kura zote katika uchaguzi mkuu kuliko mgombea mwingine wa urais katika uchaguzi mkuu uliopita.

Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu, ameyasema hayo wakati na kuongeza kuwa Lowassa aliongoza wagombea wote katika utafiti maalum uliofanywa na shirika moja kutoka nchi za nje na kuonesha kuwa anakubalika na watanzania walio wengi.

“Wazungu wakatuambia hivi political personalities zote za Tanzania walimfanyia kila mmoja wao walimfanyia uchunguzi wake, wakatuambia hivi ‘katika wote hao ukimweka huyu na huyu, huyu bwana mkubwa Lowassa huyu yeye peke yake anatembea na asilimia 18 ya Tanzania voters,’ aliyekuwa anamfuata alikuwa na asilimia 11 tu. Kwahiyo Lowassa as Lowassa alikuwa na eighteen percent ya likeability ya kupendwa na hao Watanzania akienda huku anaenda na asilimia 18 ya ziada, akienda huku anaenda na asilimia 18 za ziada nyingine ongezeeni,” amesema Lissu.

“Tukasema hivi, ‘tunataka kushinda uchaguzi eeh tuzungumze na Lowassa’ na Dkt Slaa akasema tuzungumze na Lowassa tukamwambia ‘Dkt una mawasiliano naye’ akasema ‘sina mawasiliano naye, ila kuna mtu ambaye anaweza akawezesha mawasiliano naye ni nani? Askofu Gwajima’ tunaelewana, so this how we got Edward Lowassa,” amefafanua Lissu.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni