Habari/News

Lissu afichua kama ataendelea kutoa msaada wa kisheria

Tarehe December 5, 2017

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu akiwa hospitalini Jijini Naiobi.

Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Tundu Lissu ametumia maadhimisho ya wiki ya msaada wa sheria kuwaomba wananchi kumuombea apone na kurudi nchini ili aendelee kutoa mchango wake katika taaluma ya sheria.

Mwakilishi wa Chama cha Wanasheria Tangnyika (TLS), John Seka amesema hayo katika ufunguzi wa wiki ya msaada wa Sheria na kudai kuwa Lissu anawasalimia wananchi.

“Rais wa TLS, Tundu Lissu anawasalimia sana, anaendelea kupata nafuu ila anawaomba Watanzania waendelee kumwombea ili apone haraka,” amesema Seka.

Amesema Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) ana hamu ya kurudi nyumbani aendelee kutoa mchango wake wa kisheria kwa wananchi.

Seka ametoa wito kwa wananchi kufika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam na mikoani kupata huduma ya msaada wa kisheria.

Amesema baada ya wiki hiyo kumalizika, wananchi watatakiwa kufika ofisi za TLS kupata msaada wa kisheria kwa kuwa hilo ni moja ya majukumu ya chama hicho.

Kuanzia Desemba 4 hadi 8, 2017, wananchi watapata fursa ya kupata msaada wa kisheria katika migogoro inayowakabili.

Lissu amelazwa katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya anakopatiwa matibabu baada ya kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi akiwa katika makazi yake Area D Mjini Dodoma, Septemba 7, mwaka huu.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni