Habari/News

Lipumba ‘azikwepa’ Milioni 300 za Ruzuku CUF

Tarehe January 12, 2017

Prof Ibrahim Lipumba.

Prof Ibrahim Lipumba.

 

Mwenyekiti wa chama cha CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahimu Lipumba amekwepa kuzungumzia sakata la kukizunguka chama cha CUF na kuchukua milioni 300 fedha za ruzuku.

Akiwa kwenye kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi wa Diwani wa Kata ya Kiwanja cha Ndege mjini  Morogoro Lipumba alidai kwamba CUF ndiyo chama cha siasa kinachoweza kupambana na mafisadi, dhuluma na uonevu na siyo vyama vingine.

Kwenye mkutano huo baadhi ya wananchi na wananchama wa CUF walitegemea kiongozi huyo aliyepo kwenye Mgogogro na chama chake angetoa kauli kuhusiana na tuhuma za kukwapua fedha hizo kutoka Hazina.

Aidha, Profesa Lipumba aliongeza kuwa  CCM na Chadema haviwezi kupambana na ufisadi kwa sababu bado vina baadhi ya viongozi waliowahi kutuhumiwa kuhusishwa na ubadhirifu.

Kwa upande mwingine amewataka wakazi wa kata hiyo kumchagua mgombea udiwani kupitia chama hicho, Abeid Mlapakolo ili alete mabadiliko ndani ya kata yao.

Hivi karibuni Kambi inayoongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba imechukua Sh369.4 milioni kutoka serikalini ikiwa ni mgawo wa ruzuku ya chama hicho suala linalopingwa vikali na kambi ya Maalim Seif ambaye ni Katibu Mkuu wa Chama hicho.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni