Habari/News

Lema, Jerry Muro wazidisha utata safari ya Mnyika kwenda CCM

Tarehe December 5, 2017

Mbunge wa Kibamba kwa tiketi ya Chadema, John Mnyika.

Licha ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kukaririwa mapema leo kikikanusha fununu zilizozagaa mitandaoni zikielekeza kuwa Mbunge wa Kibamba (Chadema), Mhe. John Mnyika anatazamiwa kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM), bado ishara zimezidi kuonesha kuwa safari ya kinara huyo wa upinzani kuelekea CCM imezidi kuiva.

Tetesi hizo zimegonga vichwa vya mitandao ya kijamii jioni hii baada ya kada wa CCM, Jerry Muro kutumia mtandao wa kijamii wa Instagram kwa kuweka picha ya Rais, Dkt. John Pombe Magufuli na John Mnyika na kuandika maneno kadhaa kama ifuatavyo;

“Wanakuita mvulana, basi nenda kwa Baba ukadeke kidogo kule ulikua unakomazwa tu, #safarimojamatata.”

Wakati wengi wakitafakari maneno ya Jerry Muro, Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema) naye ametumia mtandao wa kijamii kuandika machache yaliyotafsiriwa kama maneno yanayoongelea sakata la Mnyika kutimkia CCM. Lema ameandika yafuatayo;

“Kikao kingine kitafanyika usiku huu, Mbunge mmoja kutoka Kaskazini na viti maalumu kutoka pwani, habari kamili kesho,” ameandika Lema.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni