Habari/News

Lema amrushia ‘dongo’ Masha baada ya kujitoa Chadema

Tarehe November 15, 2017

Godbless Lema akisalimiana na Lawrence Masha.

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ametumia mtandao wake wa kijamii wa Twitter kumrushia ‘dongo’ aliyekuwa mwanachama wa Chadema aliyehamia hivi karibuni, Lawrence Masha baada ya kuamua kujivua uanachama katika chama hiko kikuu cha upinzani.

Masha ambaye awali alikuwa mwanachama wa CCM na Waziri wa Mambo ya Ndani wa zamani, alitumia siku ya jana kutangaza kujivua uanachama wa Chadema akiainisha sababu tano za kufanya hivyo ikiwemo kujiridhisha kwake pasipo shaka kuwa upinzani wa sasa nchini hauna nia wala sababu ya kutafuta fursa ya kuunda Serikali kupitia falsafa, sera na uongozi mbadala.

Muda mchache baada ya Masha kutangaza maamuzi yake, Lema aliamua kutumia mtandao wa Twitter kusema machache ya moyoni kama ifuatavyo;

“Lawrence Masha, struggle ya kupigania usawa, haki na demokrasia ni safari ndefu na ngumu, wavulana wengi wameendelea kushindwa vile vile wanaume na wanawake imara wanaendelea na safari, sio uamuzi mbaya uliouchukua ila ni uamuzi wa aibu. Utajua baadae na sio sasa.”

Hili linajiri wakati kada mwingine wa CCM na aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amehama kutoka CCM na kuingia Chadema kwa madai kuwa Serikali ya CCM imepoteza muelekeo wake.

Viongozi wengine wakubwa waliohama CCM na kwenda Chadema ni pamoja na Mawaziri Wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Fredrick Sumaye.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni