Habari/News

Lema afunguka Magufuli kukutana na Bosi ACACIA

Tarehe June 15, 2017

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.

Mbunge wa Arusha Mjini Bw.Godbless Lema amefunguka kuhusiana na Rais Magufuli kukutana na Bosi kampuni ya madini ya ACACIA ambaye amekubali kulipa fedha zote kampuni hiyo inazodaiwa toka ianze kuchimba madini hapa nchini.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli  alisema jana kuwa  amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mmiliki mkubwa wa kampuni ya Acacia Mining Limited Prof. John L. Thornton  Ikulu jijini Dares salaam.

Baada ya Mazungumzo hayo Prof. John L. Thornton amesema kampuni yake ipo tayari kufanya mazungumzo na Tanzania yatakayozingatia maslahi ya pande zote mbili na pia ipo tayari kulipa fedha zote ambazo inapaswa kulipa kwa Tanzania.

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii Lema amesema amependa Rais alivyokutana na Bosi wa Acacia na kufanya nae mazungumzo kwa upole na kufikia muafaka wa kuilipa serikali madeni yote.

 

Screenshot_20170614-235506-768x341 (1)

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni