Tarehe June 13, 2017

Sehemu ya Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Kikosi cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kimepelekwa Mkoani Pwani kwa ajili ya kudhibiti na kutafuta wahalifu ambao wamekuwa wakifanya mauaji kwa muda mrefu sasa mkoani humo katika maeneo ya Kibiti, Ikwiriri na Mkuranga.
Kikosi hicho kina wanajeshi wenye uzoefu mkubwa wa kivita na makomandoo huku lengo likiwa ni kuleta amani na kukomesha mauaji hayo ambayo kwa kipindi kirefu yamekuwa yakihatarisha maisha ya wakazi wa Pwani na kuharibu mfumo mzima wa maisha yao.
Katika kuhakikisha mauaji hayo yanatokomezwa, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro alitangaza ‘bingo’ ya Shilingi Milioni Kumi (10) kwa yeyote atakayetoa taarifa kuhusiana na wahalifu hao na kulisaidia Jeshi hilo kuwatia nguvuni
Maoni