Habari/News

Serikal yaagiza Takukuru, polisi kumchunguza Nyalandu

Tarehe November 13, 2017

Mhe. Lazaro Nyalandu.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla amesema mmoja wa mawaziri wa zamani katika wizara hiyo, Lazaro Nyalandu alitumia vibaya madaraka yake na kuikosesha Serikali mapato ya zaidi ya Shilingi bilioni 32.

Waziri Kigwangalla amesema hayo bungeni alipokuwa akichangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/2018 na kuitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa kushirikiana na polisi kumchunguza Nyalandu.

“Nyalandu aliikosesha Serikali mapato ya Shilingi bilioni 32 kwa miaka miwili aliyohudumu katika Wizara ya Maliasili kwa kushindwa kusaini sheria ya tozo kwa hoteli za kitalii,” amesema Waziri Kigwangalla.

Aidha, Kigwangalla amesema Nyalandu alikuwa akitumia ndege aina ya ‘Helicopter’ ama Chopa ya mwekezaji mmoja raia wa kigeni wakati wa kampeni za kugombea tiketi ya kuwania urais mwaka 2015, ambaye kampuni yake ilikuwa ikituhumiwa kwa ujangili.

Hivi karibuni Nyalandu ambaye alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini alijiuzulu ubunge wake na kujivua nyadhifa zake zote ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kutangaza nia ya kuhamia Chadema ambapo tayari amekwishapokelewa kwa mikono miwili.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni