Habari/News

Kenyatta atoa ya moyoni kuuawa Wanajeshi 15 wa Tanzania nchini DRC

Tarehe December 11, 2017

Rais Dkt John Pombe Magufuli, akiwa na Rais wa Kenya, Mh. Uhuru Kenyatta.

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amemuandikia barua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wa Tanzania.

Katika barua hiyo Rais Kenyatta  amepinga kitendo cha mauaji ya askari wake 15 waliokuwa wakilinda amani nchini Kongo, na kumpa pole kufuatia msiba huo mkubwa.

Rais Kenyatta amesema kushambuliwa kwa askari, ambao walikuwa wakihudumia kwa sababu nzuri ya kuanzisha amani ya kudumu nchini DRC ilikuwa mbaya, huku akiwapa pole watanzania na ndugu wa marehemu, na kuwaombea wale waliojeruhiwa waweze kupona haraka.

Ameongeza kuwa Kenya itaendelea kushirikiana na watu na serikali ya Tanzania katika kulinda amani ya Kongo na maeneo ya maziwa makuu, na kuangalia kesho bora ya maeneo hayo.

Rais Kenyatta amesema Kenya inathamini jukumu muhimu lililofanywa na watunza amani tangu imehusika katika mipango mingi ya kulinda amani.

Barua ya Kenyatta inafuatia   wiki iliyopita askari 15 wa Tanzania waliokuwa wakilinda amani nchini Kongo waliuawa na askari waasi wanaoendesha mapigano nchini humo. huku 44 wakijeruhiwa, 8 wakiwa mahututi na wawili hawajulikani walipo.

Kwa upande   muwakilishi wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania (CDF) Luteni Jenerali James Mwakibolwa alisema tukio hilo halitawavunja moyo na kamwe Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania halitatetereka kupeperusha bendera yake ndani na nje ya nchi kwani tukio hilo limewaongezea nguvu, ari ,ushupavu na uhodari zaidi katika kutekeleza majukumu yake.

Kuhusu taratibu za kusafirisha miili ya marehemu kuirejesha nchini alisema  zinafanyika chini ya utaratibu wa Serikali na umoja wa Mataifa na JWTZ na Serikali wanaendelea kuchukua hatua stahiki kufuatia tukio hilo.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni