Habari/News

Kenyatta ‘ambwaga’ Odinga Urais Kenya

Tarehe August 12, 2017

Uhuru Kenyatta.

Uhuru Kenyatta.

 

Hatimaye,Tume ya taifa ya uchaguzi Kenya imemtangaza Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Kenya.

Rais Kenyatta alipata kura 8, 203, 290 ambayo ni asilimia 54 naye mpinzani wake mkuu, mgombea wa muungano wa upinzani wa National Super Alliance Raila Odinga  ambaye  amepata kura milioni 6,762,224 ambayo ni asilimia 44.

Akitangaza matokeo hayo mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC Wafula Chebukati alisema kuwa ni asilimia 78 ya wapiga kura milioni 19 waliosajiliwa pekee walioshiriki uchaguzi huo.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni