Habari/News

Kauli ya Nape yazua utata,ni kuhusu ‘Vyuma vimekaza’

Tarehe December 22, 2017

 

Mbunge wa jimbo la Mtama kwa tiketi ya (CCM) Nape Nnauye.

Msemo wa Vyuma ‘vimekaza umeendelea kushika kasi mitandoni licha ya Rais Dkt.John Pombe Magufuli kupiga marufuku msemo huo unaomaanisha  kwamba hali ni mbaya ya kiuchumi kwa wananchi.

Aidha,Mbunge wa jimbo la Mtama kwa tiketi ya (CCM) Nape Nnauye amechapisha ujumbe unaoleta utata huku baadhi ya watu wakiutafsiri kuwa ujumbe huo unamaanisha vyuma vimekaza.

“Ni rahisi kuchukulia poa kwasababu kwako mambo yanaenda, lakini sio hata kidogo”Ameandika Nape katika Instagram yake.

Watu mbalimbali wametoa maoni yao ambapo wengine wamemtaka Mbunge huyo kuweka wazi kuwa hali ni mbaya kwa sababu wao ndio wawakilishi wa Wananchi Bungeni

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni