Habari/News

Kauli ya Naibu waziri Ulega juu ya Maofisa wa Forodha ya Sirari

Tarehe November 2, 2017

Abdallah Ulega Naibu Waziri Mifugo na Uvuvi Akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mra Adamu Malima

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi  Abdallah Ulega amewataka Maofisa wa Forodha ya Sirari Wilayani Tarime kuongeza juhudi katika kulinda rasilimali ili kuunga mkono juhudi za rais Dk. John Magufuli ya kulinda rasilimali za Taifa.

Waziri Ulega amayasema hayo wakati akizungumza na wafanyakazi wa forodha hiyo katika kikao na watendaji wakati wa ziara yake katika eneo hilo.

Aidha katika ziara yake pia Ulega amepata nafasi ya kuzungumza na mkuu wa mkoa wa mara Adamu Malima ambapo wamekukubaliana kudhibiti uvuvi haramu hasa unaofanyika katika ziwa Victoria na kwa upande wake Malima ameahidi kuwa atahakikisha anatumia vyombo vya dola kukabiliana na hali hiyo.

Viongozi hao wamekubaliana pia kuanza mchakato wakufufua viwanda vya kusindika samaki na nyama vilivyopo ili kuunga mkono juhudi na jitihada za Mh. Rais Dk. Magufuli za kuwa na Tanzania ya viwanda.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni