Habari/News

Kauli ya Kingunge kwa Rais Magufuli

Tarehe January 6, 2018

Rais John Pombe Magufuli alipomjulia hali Mzee Kingunge Ngombale Mwiru Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Rais John Pombe Magufuli amemjulia hali Mzee Kingunge Ngombale Mwiru  aliyelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Mzee Kingunge anatibiwa majeraha baada ya kushambuliwa na mbwa, akiwa katika kitanda cha hospitali amemwambia rais Magufuli  kuwa CCM ni chama chake na amekiunda yeye.

“CCM ni chama changu nimetoka tu, tumeachana lakini nimefanya kazi zote, nimekiunda mimi, hakiwezi kuwa kinyume changu,”– Mzee Kingunge

Kingunge alitangaza kuachana na chama cha Mapinduzi (CCM)kufuatia kutoridhishwa na mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya CCM ambapo Dkt John Magufuli aliteuliwa na Mwanasiasa Edward Lowassa kukatwa.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni