Habari/News

Kauli ya Kikwete Mama Samia kumjulia hali Tundu Lissu

Tarehe November 29, 2017

Makamu wa Rais Samia Suluhu alipo mjulia hali Mwanasheria Mkuu Chadema Tundu Lissu.

Mbunge wa Chalinze kupitia CCM ambaye pia ni mtoto wa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ameonesha kufurahishwa na kitendo cha Makamu wa Rais kumjulia hali Mwaasheria mkuu wa Chadema Tundu Lissu aliyepigwa risasi mjini Dodoma.

Makamu wa Rais mama Samia Suluhu jana  alikwenda hospitali nchini Kenya  kumuona Tundu Lissu ambaye amelazwa tangu Septemba 7 mwaka huu, baada ya kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Ridhiwani Kikwete ameandika ujumbe akisema kuwa Mama Samia ameonesha kuguswa kama mzazi kwa kitendo alichokifanya cha kwenda kumuona mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antiphas Lissu.

“Sura yake Makamu wa Rais Mama Samiah Hassan inaonyesha kuguswa kama Mzazi. Wewe ni mzazi na Mungu aibariki Tanzania”, ameandika Ridhiwani.

Mama Samia anakuwa Kiongozi wa kwanza ngazi ya juu kumjulia hali Mbunge huyo tangu alazwe hospitalini kutokana na kupigwa risasi na watu wasiojulikana

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni