Habari/News

Kashililah afafanua sintofahamu uteuzi wa Katibu Mpya Bunge

Tarehe October 8, 2017

Dkt. Thomas Kashililah.

Katibu wa Bunge wa zamani, Dkt. Thomas Kashililah amesema, Rais, Dkt. John Pombe Magufuli hakufanya kosa katika uteuzi wa Katibu wa Bunge na kwamba hakuna shria yoyote iliyovunjwa.

Dkt. Kashililah amenukuliwa akisema kuwa kwa mujibu wa ibara ya 87(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano  mamlaka ya uteuzi haikufanya kosa licha ya sheria ya Bunge kuelekeza utaratibu.

“Mamlaka ya uteuzi iko sahihi. Unajua sheria haiko juu ya Katiba na Katiba iko juu ya sheria, hivyo Rais akiamua anaweza kufanya hilo, sheria haiwezi kumzuia,” amesema Dkt. Kashililah akisisitiza ibara ya 87 iko wazi ambayo inasema “Kutakuwa na Katibu wa Bunge ambaye atateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye madaraka ya juu katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano.”

Ameongeza kuwa kama aliyeteuliwa asingekuwa katika madaraka ya juu, hapo kungekuwa na tatizo, lakini mteule ni mtu ‘senior’ kabisa Serikalini na hivyo ana vigezo vyote na kuwataka watu kuacha kupotosha ukweli.

Rais Magufuli jana Jumamosi alimteua, Steven Kagaigai kuwa Katibu wa Bunge huku Dkt. Kashililah akidaiwa kuwa atapangiwa kazi nyingine.

Mara tu baada ya uteuzi huo, mijadala ilianza katika mitandao ya kijamii kuhusiana na uhalali wa Rais kufanya uteuzi huo, ambapo Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe akienda mbali zaidi na kudai kuwa Rais amevunja sheria kwa kufanya hivyo na tayari chama chake kimetishia kwenda mahakamani kupinga uteuzi huo kama Rais hatoutengua.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni