Habari/News

Kampuni ya Mwananchi yaomba msaada kupatikana kwa mwandishi wake

Tarehe December 7, 2017

 

Uongozi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji, Francis Nanai umeiomba Serikali kusaidia kupatikana kwa mwandishi wake wa kujitegemea, Azory Gwanda anayedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana ( ).

Amesema mwandishi huyo hajaonekana ikiwa ni siku ya 17 tangu kuchukuliwa na watu waliokuwa katika gari nyeupe baada ya kufanya upekuzi katika nyumba yake.

Kwa mujibu wa Nanai, wamefatilia tukio hilo katika kituo cha polisi lakini hadi leo hawajapata taarifa yoyote.

Amesema tukio lolote kwa mwandishi wa habari ni sawa na kuingilia uhuru wa vyombo vya habari na kwamba tukio la kuteka kwa mwandishi huyo ni mojawapo wa matukio hayo.

“Itapendeza sana kama tutaendelea kupata ushirikiano kutoka vyombo vya habari na mashirika mengine ya kutetea haki za binadamu kuhusiana na tukio hilo,” amesema.

Aidha, amesema kuwa Kampuni hiyo itaendelea kuwa karibu na familia ya Azory Gwanda hadi pale atakapopatikana.

Naye Mwakilishi kutoka Jukwaa la Wahariri, Theophil Makunga amesema kuwa kuna nia ovu katika kukamatwa na kutekwa kwa mwandishi huyo kwani kama alikuwa amefanya kosa la kijinai alipaswa kuwa ameshafikishwa katika vyombo husika.

 

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni