Habari/News

Kampuni 57 zatajwa kushindwa kuwasilisha makato ya Wadaiwa Sugu

Tarehe January 6, 2018

Hatimaye Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) imetaja  majina 57 ya kampuni, shule, vyuo na mashirika ambayo waajiri wake hawawasilishi makato ya wanufaika wa mikopo kwa wakati kama inavyotakiwa.

Kwa mujibu wa  Mkurugenzi Msaidizi Urejeshaji Mikopo, Phidelis Joseph alisema kabla ya kuanza kuwasaka wanufaika 119,497 ambao hawajarejesha mikopo yao, wataanika majina yao hadharani.

Miongoni mwa kampuni zilizotajwa ni pamoja na Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco), Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Shirika la NSSF, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Puma Energy Limited, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).

Uanikaji wa majina hayo kupitia tovuti ya HESLB umekuja siku mbili baada ya kutangaza kufanya hivyo Jumatano iliyopita.
 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni