Habari/News

Kada wa zamani Chadema aula Baraza jipya la Mawaziri

Tarehe October 7, 2017

Juliana Shonza

Kada wa zamani wa Chadema maarufu kama Juliana Shonza ameula kufuatia kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenye Baraza jipya la Mawaziri Serikali Dkt.John Pombe Magufuli.

Shonza anachukua nafasi iliyo achwa ya Annastazia Wambura aliye enguliwa na Rais Magufuli wakati akitangaza Baraza jipya la Mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo.

Shonza ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum CCM alihama chama cha Demokrasia na maendeleo mwaka 2013 kwa madai ya chama hicho kutumia vijana vibaya ili kufanya fujo.

Hivi karibuni Shonza ali ingia  kwenye  mvutano na wabunge wa chama chake cha zamani chama cha Chadema.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni