Afya

Jaribio la kifaa kinachowalinda wanawake dhidi ya HIV lafanikiwa

Tarehe July 26, 2017

DAWAA

Watafiti nchini Marekani wamesema kuwa jaribio ambalo vijana wa kike walitumia mpira wa mviringo kujilinda na virusi vya HIV, limefanikiwa.

Wasichana hao walitumia mviringo wa plastiki uliowekwa dawa za kujilinda na ugonjwa wa ukimwi, ambao ulibadilishwa kila mwezi katika kipindi cha miezi sita.

Jaribio hilo ni mojawapo ya mipango ya kutengeneza kifaa ambacho wanawake watatumia kujilinda dhidi ya maambukizi ya HIV na kuondoa utegemezi kwa wanaume kuvaa mipira ya kondomu.

Watafiti hao wamesema kuwa wanafurahi kwamba wasichana waliotumia mviringo huo wameupenda.

Wanawake na wasichana walio kati ya umri wa miaka 15-24 wanadaiwa kuwa sehemu kubwa ya maambukizi ya HIV duniani huku takriban wanawake 1000 huambukizwa virusi hivyo kila siku kusini mwa Jangwa la Sahara Barani Afrika.

Utafiti zaidi wa mpira huo wa mviringo unatarajiwa kufanywa kwa vijana barani Afrika.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni