Habari/News

IMF yaanika Hali halisi ya uchumi Tanzania

Tarehe January 14, 2018

Benki kuu ya Tanzania

Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limesema  Serikali ya Tanzania inafaa kuchukua hatua za haraka ili kubadilisha mwelekeo wa kushuka  kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

Kupitia taarifa yake mpya kuhusu uchumi wa Tanzania, IMF imesema kuwa, licha ya kuwa takwimu za pato la taifa kuonyesha kukua, lakini takwimu nyingine za uchumi zinaeleza kudorora kwa shughuli za kiuchumi.

Aidha,imebainisha kuwa  ukusanyaji wa mapato umekuwa mdogo kuliko ulivyotarajiwa na ongezeko la alama za imani limekwama katika baadhi ya mabenki kutokana na kuongezeka kwa mikopo mibaya.

Kumekuwa na athari mbaya kwenye ukuaji wa uchumi katika kipindi kifupi kutokana na utekelezaji mdogo wa bajeti, ulioleta changamoto kwenye mazingira ya kibiashara, na sekta binafsi ikilalamika kubanwa sana na sheria.

Uchumi wa Tanzania katika kipindi cha muongo mmoja uliopita ulikuwa unakua kwa asilimia 7 kwa mwaka, lakini mwezi Novemba Benki ya dunia ilitangaza kuwa kasi hiyo huenda ikapungua hadi asilimia 6.6 mwaka jana

Taarifa hiyo imetolewa baada ya kukamilisha mapitio yake ya Sera za Kukuza Uchumi PSI kuhusu Tanzania.

Hata hivyo wanasiasa mbalimbali akiwemo Zitto Kabwe na Hussein Bashe wamewahi kuhoji kuhusu uchumi kushuka  hata hivyo Serikal ilipinga na kudai kuwa uchumi umekua ukikua kila kukicha.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni